Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mwana wa aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni (Israel), Naftali Bennett, ndiye mtu wa hivi karibuni kuwasilishwa kimakosa na baadhi ya vyombo vya habari (vya maadui) kama miongoni mwa waandamanaji waliodaiwa kuuawa na vikosi vya usalama vya Iran.
Kwa mujibu wa PressTV, hatua hiyo ni sehemu ya kampeni ya upotoshaji, ambapo picha za watu wasiokuwa na uhusiano na matukio ya Iran hutumiwa kuunda simulizi za uongo kuhusu hali ya ndani ya nchi hiyo.
Ripoti zinaeleza kuwa matumizi ya picha za watu wa nje kama “waathirika wa Iran” ni mbinu ya kupotosha umma na kuchochea hisia za kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Your Comment